Dodoma.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema Serikali imezuia watu kufanya biashara ya mazao kwa kupeleka nnje ya nchi kinyume na utaraibu. Bashe amesema hayo alipokuwa akizindua ofisi ya kuleta mabadiliko ya sekta ya kilimo nchini jijini Dodoma Jumatatu Juni 19, 2023 ambapo ameeleza kuwa Serikali haitaruhusu mtu yeyeyote kusafirisha mazao nje ya nchi ikiwa hajasajili kampuni, hana Tin namba, taarifa za ulipaji kodi pamoja na leseni ya biashara husika.
Bashe amesema kuwa Serikali iliamua kurasimisha shughuli za kilimo hivyo zinatafsiriwa kama shughuli nyingine kwani nchi inataka kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato.
Ameendelea kusema Serikali haikupiga marufuku usafirishaji mazao nje ya nchi kwa biashara, bali imezuia kufanya hivyo bila kufuata utaratibu.
“Marufuku inayosemwa kwenye kusafirisha nje, ni kwa mazao yote ya kilimo ikiwemo chakula kwa wafanyabishara wasiofuata utaratibu.
"Utaratibu unaotakiwa kufuatwa na mfanyabiashara ni kusajili kampuni yake hapa nchini, awe amekata leseni ya kusafirisha mazao nje ya nchi, awe na namba ya utambulisho ya mlipakodi (TIN) na awe na leseni ya biashara," alisema Bashe.
Kauli hiyo inakuja baada ya mkwamo wa siku kadhaa wa malori 120 yenye shehena ya mahindi eneo la Himo mkoani Kilimanjaro kuelekea Kenya ambayo mkuu wa mkoa huo, Nurdin Babu alitaka yarudishe mzigo huo na kuuza nchini kutokana na kuwa na vibali stahiki.
Chanzo: Gazeti la mwananchi
MAONYESHO YA KIMATAIFA YA NAIROBI (NAIROBI INTERNATIONAL TRADE FAIR)
Read MoreKONGAMANO LA KIBIASHARA KATI YA TANZANIA NA SUDANI KUSINI YAFUNGUA MILANGO YA BIASHARA
Read MoreTANZANIA NA UGANDA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA
Read More