East Africa Business News

KONGAMANO LA KIBIASHARA KATI YA TANZANIA NA SUDANI KUSINI YAFUNGUA MILANGO YA BIASHARA

Naibu Waziri wa fedha na Mipango wa Serikali ya Sudani Kusini Mhe. Agog Makur amefungua rasmi kongamano la kibiashara la biashara kati ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na wa Sudan Kusini kwa lengo la kuvumbua fursa za kibishara zilizopo nchini Sudani Kusini ambapo zaidi ya mashirika na wafanyabiashara 70 wameshiriki katika hotel ya Radisson Blue Hotel, Juba.
Mhe. Makur amesema nchi ya Sudani Kusini ina fursa nyingi katika maeneo ya Kilimo, viwanda, afya, sayansi na teknolojia, Elimu pamoja na mafuta ambazo zinaweza kutumiwa na Tanzania na kukuza uchumi wa pande zote mbili.
“Ninayofuraha kubwa kuwa hapa siku ya leo kufungua kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na nchi yetu ya Sudani Kusini, leo historia imeandikwa ambapo ushirikiano kati ya Tanzania na Sudani kusini katika sekta mbalimbali unakwenda kuimarishwa mara dufu, karibuni sana na jisikiane mko nyumbani” Alisema Mhe. Makur
Balozi wa Tanzania Nchini Kenya anayesimamia nchi ya Sudani Kusini Mhe. Dr. John Simbachawene amesema Kongamano la kwanza la kibiashara kati ya Tanzania na Sudani kusini litaleta tija kubwa kwani ni muda muafaka wa wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali za Tanzania kutumia fursa ya soko lililopo katika nchi ya Sudani kusini.
“ Kwakuwa nchi hii ya Sudani Kusini ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki naomba niwahakikishie kwamba hawa ni ndugu zetu kama zilivyo nchi nyingine za Jumuiya yetu, hivyo niwaombe wafanyabiashara na Taasisi mbalimbali kutoka Tanzania kukaa na wenzetu hapa Sudani kusini ili kuona namna bora ya kutumia fursa hizo kwa manufaa ya nchi zetu zote mbili” Alisema Mhe. Dr. John Simbachewene.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Tantrade Prof. Ulingeta O.L. Mbamba amesema wameandaa msafara wa kibishara nchini Sudani ili kuangazia fursa zilizopo na kuwapa fursa hizo wafanyabiashara kutoka Tanzania ili waweze kulifikia kiurahisi soko la nchini Sudani Kusini ambalo bado Tanzania haijanufaika nalo.
“ Leo tuko hapa Sudani Kusini katika msafara wa kibishara ambao sisi Tantrade kwa kushirikiana na wenzetu wa Ofisi ya ubalozi wa Tanzania nchini Kenya tumeratibu msafara huu kwa lengo la kufungua milango ya kibishara na sekta nyingine kati yetu Tanzania na nchi hii ya Sudani Kusini, tunafanya kongamano ambalo limeleta pamoja wafanyabishara wa Sudani Kusini na wa Tanzania, naamini baada ya kongamano hili nchi zetu mbili zitanufaika na ushirikiano utakaoanza” Alisema Prof. Mbamba
Kongamano la Kibiashara kati ya Tanzania na nchi ya kusini linafanyika kwa siku mbili katika mji wa Juba ambapo wafanyabiashara, Taasisi na mshirika mbalimbali kutoka nchi zote mbili yanashiriki kwa lengo la kujengeneana uelewa wa pamoja juu ya fursa zilizopo kwenye nchi zote mbili na kuangalia namna bora ya kuzitumia fursa hizo.

Chanzo: Tantrade

 

Related Articles

East Africa Business News | 11-09-2022

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA NAIROBI (NAIROBI INTERNATIONAL TRADE FAIR)

Read More
East Africa Business News | 11-05-2023

TANZANIA NA UGANDA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA

Read More
East Africa Business News | 21-05-2023

KENYA KUTOA GHALA KWA WAUZA NAFAKA WA TANZANIA

Read More