East Africa Business News

TANZANIA NA UGANDA KUONDOA VIKWAZO VYA BIASHARA

TANZANIA na Uganda zimekubaliana kuondoa vikwazo vya biashara, ili kuendeleza na kuboresha ushirikiano kati ya mataifa hayo kwenye nyanja mbalimbali.


Makubaliano hayo yamefikiwa katika mkutano wa majadiliano kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Stergomena Tax  na Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza wa Uganda na Waziri anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki,  Rebecca Kadaga uliofanyika katika ofisi ndogo za wizara jijini Dar es Salaam.


Katika mkutano wao, viongozi hao wamekubaliana kukamilisha michakato ya kuendeleza miundombinu, ili kukamilisha barabara zinazounganisha Uganda na Tanzania, usafiri katika ziwa Victoria ambao pia utaunganisha reli ya kisasa ya SGR kwenda Uganda.


“Tumewekeana muda ili tuweze kukamilisha baadhi ya masuala kwa haraka, lakini pia kuona jinsi gani pale panapohitaji kila nchi itoe rasilimali iweze kujipanga na kuhakikisha rasilimali hizo zinapatikana kwa wakati,” alisema Dk Tax.


Katika mkutano huo viongozi hao wamekubaliana pia kukamilisha ujenzi wa kituo cha uokoaji jijini Mwanza kitakachoshughulikia maafa yanayoweza kutokea katika ziwa Victoria.

Related Articles

East Africa Business News | 11-09-2022

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA NAIROBI (NAIROBI INTERNATIONAL TRADE FAIR)

Read More
East Africa Business News | 24-03-2023

KONGAMANO LA KIBIASHARA KATI YA TANZANIA NA SUDANI KUSINI YAFUNGUA MILANGO YA BIASHARA

Read More
East Africa Business News | 21-05-2023

KENYA KUTOA GHALA KWA WAUZA NAFAKA WA TANZANIA

Read More