Kabla ya kusajili Jina la Biashara, lazima uwe umekidhi vigezo vifuatavyo:-
1) Kufungua akaunti katika ORS lazima uwe na nambari ya utambulisho wa utaifa (NIN) inayotolewa na NIDA.
2) Mmiliki wa Jina la Biashara lazima awe na nambari ya utambulisho wa utaifa (NIN) inayotolewa na NIDA.
Tembelea Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao kwa anwani ya wavuti https://ors.brela.go.tz/ors au kwa kutembelea tovuti ya BRELA: www.brela.go.tz na chagua “BUSINESS NAMES ONLINE REGISTRATION”
Kama huna akaunti kwenye mfumo wa ORS, bofya "Tengeneza Akaunti ya ORS" na ikiwa una akaunti tayari, ingia kwenye mfumo kwa kutumia jina lako la mtumiaji na nenosiri.
Bonyeza “Anza” na kisha “Huduma mtandao”
Chagua Jina la Biashara.
Katika aina ya huduma, chagua "Usajili wa Jina Jipya la Biashara" na kisha bofya "Endelea"
Katika aina ya jina la biashara, chagua aina. mfano "binafsi" na bofya "Endelea"
Katika Fomu ya Usajili, jaza sehemu zote zilizowekewa nyota (*) ya rangi nyekundu.
Kwa kila hatua, kumbuka bonyeza "Hifadhi" ili kuhifadhi taarifa zako ili kuepuka kupoteza taarifa.
Katika sehemu ya Mwombaji, jaza Taarifa ya Uwakilishi (Mmiliki au mshiriki).
Kama mwombaji anaweza kuboresha data katika ORS bofya kitufe "anaweza kurekebisha taarifa kwenye ORS".
Katika sehemu ya “Maelezo kuhusu jina la biashara”, jaza Jina la Biashara.
Jaza taarifa zote zinazotakiwa katika sehemu ya "Ofisi ya kusajiliwa”.
Katika sehemu ya "Shughuli ya Biashara", bofya Ongeza ili kuchagua shughuli zako za biashara / malengo kulingana na Uainishaji wa “ISIC Classification” toleo la nne.
Katika sehemu ya "Umiliki", bofya “Ongeza” ili kuongeza maelezo na anwani ya mmiliki wa Jina la Biashara.
Katika sehemu ya "Mmiliki wa akaunti ya benki," jaza taarifa ya watu ambao wataendesha akaunti ya benki ya biashara.
Kwa sehemu ya "Wawakilishi," taja mtu ambaye anaweza kurekebisha taarifa katika mfumo wa ORS. Ikiwa Mmiliki / Washiriki wanaweza kurekebisha taarifa,chagua "Ndio au Hapana" ili kuwawezesha au usiwawezeshe kuwa na mamlaka ya kuwapa watu ambao wanaweza kurekebisha taarifa katika ORS, kisha kwenye eneo la “inawakilishwa mpaka”, jaza kipindi ambacho mtu huyu anaweza kurekebisha taarifa na kisha bofya "Endelea".
Subiri “consolidated form” itengenezwe.
Pakua fomu, kisha piga chapa (print) , weka sahihi pamoja na tarehe.
Pakia fomu iliyofanyiwa “Scanning” na kisha bofya "Endelea".
Katika ukurasa wa malipo, chagua njia ya kufanya malipo na kisha bofya “Kuanza malipo”. Nambari ya kulipia itazalishwa. Bofya kwenye kitufe cha “Angalia” au “Pakua” ili uone taarifa za malipo pamoja na maelekezo ya jinsi ya kufanya malipo.
Mara baada ya kufanya malipo, maombi yako yanawasilishwa kwa BRELA moja kwa moja kwa ajili ya kufanyiwa kazi.
Angalia upande wa kushoto ndani ya mfumo , bonyeza sehemu ya Maombi (Applications)
Tazama sehemu ya "Imefanyiwa kazi?" Kama ni "Yes" inammanisha ombi lako limeshughulikiwa hivyo bofya "View" kuangalia taarifa zaidi ikiwemo kuprint cheti.
Kama "Imefanyiwa kazi?" inasema "NO" na sehemu ya "Hatua ya kazi":-
Inasema "Process and Enter Recommendation" inamaanisha maombi yako BRELA na yanafanyiwa kazi.
Kama inasema "Make Final Decision", inamaanisha Maombi yako hatua ya mwisho kufanyiwa maamuzi BRELA.
HUDUMA KWA WATEJA:
0735 331 001, 0735 000003, 0735 331 00
P. O. Box 9393, Dar es Salaam - Tanzania
Tel: +255 22 218 0139, 218 1344,218 0113, 2180141,
Fax: +255 22 218 037
Barua pepe: usajili@brela.go.tz
DC Jokate Mwegelo Azindua Rasmi Tuzo Za Wajasiriamali Wa Twcc Jijini Dar
Read MoreTaarifa Kwa Mawakala Na Waagizaji Wa Bidhaa Za Chakula Na Vipodozi Nje Ya Nchi
Read MoreWaziri Bashe Atangaza Sikukuu Ya Wakulima Nane Nane Kufanyika Mwaka Huu Wa 2022
Read More