PASS leasing Company Limited ni kampuni inayomilikiwa na PASS TRUST, iliyosajiliwa Tanzania kupitia sheria za makampuni na inayoratibiwa na Benki kuu ya Tanzania. Lengo kuu la PASS leasing Company ni kusaidia sekta ya kilimo kwa kutoa mashine na zana za kilimo, uvuvi na ufugaji bila dhamana na kwa riba nafuu ili kuwawezesha wakulima kufikia malengo yao.
Huduma zinazotolewa na PASS leasing
Upatikanaji wa zana za kilimo na viwanda ikiwemo:-
1.Kilimo-Zana za kuwezesha uzalishaji wa kilimo cha mazao, umwagiliaji, usindikaji, uhifadhi na usafirishaji wa mazao
2. Uvuvi-Vifaa vya uvuvi, usafirishaji, uhifadhi, usindikaji na uchakataji.
3. Ufugaji nyuki-Vifaa mbalimbali vya kuongeza tija na thamani katika sekta ya nyuki na mazao yatokanayo na nyuki.
4. Ufugaji-Vifaa vya utunzaji wa mifugo, utengenezaji wa vyakula na mashine mbalimbali za kuongeza tija katika sekta ya mifugo.
5. Mashine zitumikazo kwenye upandaji, uvunaji. Usafirishaji na viwanda vya mbao.
Nani anaweza kunufaika na PASS leasing
1. Mtu binafsi, kikundi, chama au kampuni ilisajiliwa nchini.
2. Mwenye umri halali wa kuingia mkataba(18+)
3. Mwenye akili timamu
Sifa za mwombaji
1. Anayejishughulisha na sekta ya kilimo
2. Awe na eneo la biashara analomiliki au kukodi
3. Awe na rekodi nzuri za ukopaji kwa taasisi nyingine za fedha.
4. Awe na biashara inayoweza kuingiza faida
5. Awe na uwezo wa kufanya malipo ya awali
6. Awe na uwezo wa kuthibitisha mapato yake ya nyuma.
Jinsi ya kufanya maombi
Mwombaji atapaswa kujaza fomu ya maombi inayopatika katika tovuti ya www.passlease.co.tz.
Wakati wa maombi ni muombi ni muhimu kwa mwombaji kutoa taarifa na viambatanisho vyote muhimu vinavyohusiana na biashara yake na kifaa anachokiomba kupitia kampuni ya PASS leasing. Hii itasaidia kuharakisha mchakato wa maombi.
Mwombaji anaweza kufika katika ofisi za PASS zilizopo katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Morogoro, Mwanza, Ruvuma, Mbeya na Tabora.
Kwa maelezo zaidi piga simu
Tel: +255(0) 22 2110 394
Piga bure: 0800750037
DC Jokate Mwegelo Azindua Rasmi Tuzo Za Wajasiriamali Wa Twcc Jijini Dar
Read MoreTaarifa Kwa Mawakala Na Waagizaji Wa Bidhaa Za Chakula Na Vipodozi Nje Ya Nchi
Read MoreWaziri Bashe Atangaza Sikukuu Ya Wakulima Nane Nane Kufanyika Mwaka Huu Wa 2022
Read More